Ni kwa nini lishe bora ni muhimu kwa afya yangu
From Audiopedia
Magonjwa mengi yanaweza zuiliwa ikiwa watu wanapata chakula kizuri na cha kutosha. Mwanamke anahitaji chakula kizuri ndiposa aweze kutekeleza majukumu yake ya kila siku ili kuzuia magonjwa na kuwa na uzao wenye afya njema. Katika ulimwengu wote wanawake wengi wanaugua kutokana na lishe duni na magonjwa mengine. Lishe duni yaweza sababisha uchovu, udhaifu, ulemavu na afya mbaya kwa jumla.