Ni kwa jinsi gani naweza kuimba jiko la haybox inayopunguza moshi

From Audiopedia
Jump to: navigation, search

Hifadhi mafuta hata zaidi kwa kutumia jiko la haybox kupasha chakula au kuipika ikiwa imechemka kwenye jiko. Hii inaweza kupunguza utumizi ya mafuta kwa zaidi ya nusu unapopika maharage, nyama, mchele, au nafaka. Mchele na nafaka itatumia thuluthi moja (⅓) ya maji, kwa sababu maji kidogo itayeyuka.

Tengeneza haybox kwa kutumia sanduku la kadibodi na kwakuweka inchi 4 ya nyasi (au majani, mavazi ya zamani, manyoya, pamba au Styrofoam) kando ya sanduku. Wacha nafasi ndani ya sanduku ya sufuria yako. Kifuniko cha sanduku lazima kiitoshee.

Ukiwa unatumia jiko la haybox, kumbuka:

Chakula kinachopikwa kwenye haybox kinachukuwa muda mara 1 ½ -3 zaidi kupika kuliko chakula kinachopikwa kwa moto.

Maharage na nyama lazima kipikwe juu ya jiko lako kwa muda wa dakika 15 hadi 30 kabla ya kuwekwa katika haybox. Chakula kitahitaji kupashwa baada ya masaa 2 au 4.

Funika sufuria wakati wote na chemsha nyama tena kabla ya kuila. Hii inazuia bakteria kwa chakula chako.

Weka jiko la haybox mbali na moto wazi.


Sources
  • Burns, A. A., Niemann, S., Lovich, R., Maxwell, J., & Shapiro, K. (2014). Where women have no doctor: A health guide for women. Hesperian Foundation.
  • Audiopedia ID: sw030107