Ni jinsi gani ambavyo utupaji wa takataka unaweza kusaidia kuzuia magonjwa
Viini vinaweza kusambazwa na nzi, mende na panya, amabao makao yao huwa ni kwenye takataka kama vile masalio ya chakula na maganda ya mboga na matunda.
Ili kuzuia magonjwa, ni jambo muhimu kuweka nyumba na sehemu zilizo karibu zikiwa safi kutokana na kinyesi, takataka na majitaka. Majitaka ya pale nyumbani yanaweza kuondolewa kwa njia salama kwa kuchimba shimo au mtaro kuelekea shambani au kiwanjani.
Kemikali kama zile za kuua wadudu na magugu zinaweza kuwa hatari ikiwa hata viwango vidogo vitaingia ndani ya mahali pa kuteka maji au kwa chakula, mikono au miguu. Usioshe nguo na vyombo ambavyo hutumika katika kuchanganya kemikali karibu na mahali pa kuteka maji
Usitumie dawa za kuua wadudu na kemikali zingine pale nyumbani au karibu na chanzo cha maji. Usihifadhi kemikali karibu na au ndani ya vyombo vya kuhifadhi maji, au karibu na chakula. Usihifadhi chakula au maji kwenye vyombo vya mbolea au dawa za kuua wadudu.