Ni chakula kipi bora zaidi kwa watoto wachanga waliofikisha miezi sita
Chakula hichi ni bora kwa watoto wachanga waliofikisha miezi sita:
Chakula cha jamii (mchele, ngano, mahindi, mtama), mizizi (mihogo, viazi vikuu, viazi) na chakula wanga (ndizi na mkate).
Chakula cha protini kama nyama, kuku na maziwa lala (yaweza changanywa na vyakula vingine kama uji) Vyakula hivi ni chaguo nzuri kwa watoto waliofikisha miezi sita kwani ni rahisi kwa mtoto kusyaga ukilinganisha na maziwa ya kawaida.
Mboga na viungo kama mchicha, broccoli, chard, karoti, maboga na viazi vitamu (ambazo zinapea mwili vitamini)
Kunde, kama vile chickpeas, dengu, kunde, mbaazi, maharagwe yaliyo na umbo la figo na maharagwe lima (kuongeza aina ya chakula na kupea mwili protini na nguvu)
Mafuta haswa mafuta ya soya, mafuta mekundu ya mawese, siagi au majarini.
Mbegu kama siagi ya njugu karanga ama siagi ya nguju zingine na mbegu zilizolowa maji kama malenge, alizeti, tikiti au mbegu za ufuta (za kupa mwili nguvu na vitamini)
Ni ngumu kupatia mwili virutubisho vya kutosha kwa mtoto mchanga kama hali nyama yoyote. Hii ni kwa sababu chakula kutokana na nyama hupatia mwili virutubisho kama iron.
Mtoto anayekula lishe ya mboga anahitaji kuongezewa lishe nyingine ya dawa ya vitamin.
Madini ya chakula cha mboga haiwekwi vyema mwilini. Hata hivyo chakula chamboga kama ndegu, chickpeas ziko na madini mengi ya kutosha. Madini hayo yatatosha mwilini ikiwa vyakula hivyo vitakuliwa kwa pamoja na vyakula vilivyo na vitamin c ya kutosha kama vile machungwa na sharubati.