Mara tu unapoamua kutumia upangaji uzazi, lazima uchague mbinu. Ili kufanya uamuzi bora ni lazima ujifunze kwanza kuhusu mbinu tofauti, faida na hasara zake.
Kuna aina 5 kuu za upangaji uzazi:
Mbinu za kuzuia, ambazo huzuia mimba kuingia kwa kuzuia shahawa kufikia yai.
Mbinu za Homoni, ambazo huzuia ovari ya mwanamke kutoa yai, huwa vigumu kwa shahawa za kiume kufikia yai, na huzuilia nyumba ya uzazi kubeba mimba.
IUDs, ambazo huzuia shahawa ya mwanamume kuchanganyikana na yai la mwanamke.
Mbinu asili, ambazo husaidia mwanamke kujua wakati yuko tayari kushika mimba, ndiposa aweze kuepuka kufanya ngono wakati huo.
Mbinu za kudumu. Hii ni oparesheni inayofanywa kwa mwanamke au mwanamume na humfanya kukosa watoto kabisa baada ya oparesheni hiyo.
Sources
Burns, A. A., Niemann, S., Lovich, R., Maxwell, J., & Shapiro, K. (2014). Where women have no doctor: A health guide for women. Hesperian Foundation.