Nawezaje kuzuia shida za ukuaji na kiafya ya watoto wangu kutokana na utapiamlo
Hakikisha kuwa mtoto anakula chakula cha kutosha. Pamoja na kunyonyshwa, mtoto wa umri wa miezi 6-8 anahitaji kula kati ya mara mbili hadi tatu kwa siku na mara tatu hadi nne kwa siku kuanzia umri wa miezi 9. Unaweza pia kumpa kipande cha ndizi au mkate uliopakwa peanut butter, mara moja au mbili kwa siku. Mtoto anayechelewa kukua, au aliye na ulemavu huhitaji usaidizi wa ziada wakati wa kula.
Hakikisha kuwa mtoto anakula chakula cha kutosha. Pamoja na kunyonyshwa, mtoto wa umri wa miezi 6-8 anahitaji kula kati ya vijiko 2-3 vya hakula, ukiongezea kidogo kidogo hadi nusu kikombe kwa kila lishe. Mtoto mwenye umri wa miezi 12-23 anahitaji robo tatu hadi kikombe kimoja cha chakula kinacholiwa na familia kwa kila lishe. Watoto wenye umri wa miaka 2 kuendelea wanahitaji kikombe kimoja kwa kila lishe. Mtoto anapomaliza chakula chake na kuitisha kingine, basi unaweza kumuongezea kingine. Ikiwe ladha ya chakula fulani haimpendezi, basi mpe chakula tofauti. Mpe vyakula vipya pole pole.
Hakikisha kuwa mtoto wako anapata vyakula vya kujemga mwili na kumpa nguvu. Vyakula vinavyowasaidia watoto kukua ni kama vile maharagwe, njugu, nyama, samaki, mayai, vyakula vya maziwa, nafaka na kunde. Ni vyema pia ukiwapa vyakula vinavyotokana na wanyama. Mafuta kidogo pia yanaweza kuongeza nguvu. Mafuta yaliyotiwa vitamini ni vyanzo vizuri vya nguvu. Vyakula vinavyojenga mwili ni muhimu kwa sababu vinasaidia kuhakikisha kuwa mtoto anapata uzani na kimo kinachofaa. Vyakula vilivyohifadhiwa kwa sukari au mafuta havin avitamini wala madini na virutubisho, na huenda vikasababibisha watoto kunenepa zaidi na kukosa kimo kinachofaa.
Tahadhari sana na watoto wanaougua. Mtoto anayeugua anahitaji kupewa motisha kula vyakula vidogo vidogo mara kadhaa. Mtoto huyo anahitaji kunyonya mara kadhaa. Baada ya kuugua, mtoto anahitaji kula zaidi ya kawaida ili arudishe uzani wake na kuongeza nguvu. Ikiwa mtoto huugua kila mara, ni lazima achunguzwe na mhudumu wa afya.
Hakikisha kuwa mtoto anapata chakula kilicho na vitamini A, cha kutosha. . Maziwa ya mama yana wingi wa vitamini A. Vyakula vingine vyenye vitamini A ni maini, mayai, vyakula vya maziwa, mafuta, matunda ya rangi ya manjano na maji ya machungwa, mboga za rangi ya kijani. Ikiwa vyakula hivi havipatikani kwa viwango vinavyohitajika, mhudumu wa afya.
Ikiwa mtoto atapewa maziwa isipokuwa yale ya mama, hakikisha kuwa analishwa kutoka kwa kikombe kisafi na wala sio chupa.
Hakikisha kuwa chakula ni kisafi, lasivyo, mtoto atakuwa mgonjwa kila mara. Osha chakula kibichi na ukipike kwa kutumia maji safi. Chakula kilichopikwa lazima kiliwe siku ile ile. Kile kinachobaki, lazima kihifadhiwa vyema na kuchemshwa kwa moto wa juu.
Maji safi ni muhimu sana kwa afya ya mtoto. Maji lazima yachotwe kwenye chanzo safi na yahifadhiwe kwenye vyombo vilivyofunikwa na ni safi ndani na nje. Maji safi yanaweza kupatikana katika maeneo yaliyolindwa, kutiwa dawa, bwawa, au maji ya mvua. Ikiwa maji yanachotwa kutoka kwenye kidimbwi, mito, chemichemi, visima na matanki, lazima yasafishwe. Unaweza kuyasafisha kwa kuyachemsha, kuchuja, kuongeza klorini au kuyaweka kwenye jua.
Hakikisha kuwa haja kubwa inawekwa kwenye choo cha kuchimba au kuzikwa. Je, mikono inaoshwa kwa kutumia sabuni na maji au jivu na maji, baada ya kwenda haja? Kama hili halifanyiki, basi mtoto ataugua kila marakutokana na minyoo na magonjwa mengine. Mtoto aliye na minyoo anahitaji kupewa dawa za kuua minyoo hao kutoka kwa mhudumu wa afya.
Ikiwa mtoto huachwa peke yake, au chini ya uliinzi wa mtoto mwingine, mtoto huyo mchanga atahitaji kuangaliwa kwa makini na mtu mzima, haswa wakati wa maankuli.