Maumivu katika sehemu ya chini ya mgongo husababishwa na kukua kwa mtoto.
Namna ya kuzuia maumivu haya:
Tafuta mtu unayemwamini ili aweze kukusugua mgongo.
Zungumza na familia yako ili waweze kukusadia na kazi nzito.
Hakikisha kuwa unapoketi au unaposimama, mgongo wako uko wima.
Hakikisha kuwa unalala kwa upande na uweke kitambaa katikati ya miguu yako.
Unapohisi maumivu mgongoni, jaribu zoezi la paka aliyekasirika. Piga magoti na mikono yako pia ikiwa sakafuni. Kisha, inua mgongo wako na uurudishe chini. Rudia.
Sources
Burns, A. A., Niemann, S., Lovich, R., Maxwell, J., & Shapiro, K. (2014). Where women have no doctor: A health guide for women. Hesperian Foundation.