Nawezaje kuzuia homa ya mapafu

From Audiopedia
Jump to: navigation, search

Familia zinaweza kuzuia homa ya mapafu kwa kuhakikisha kuwa watoto wananyonyeshwa kwa miezi sita ya kwanza, na kuwa watoto wote wanapata lishe bora na chanjo zote.

Kuwanyonyesha watoto huwasaidia kuepuka kushikwa na homa ya mapafu. Ni muhimu sana kumnyonyesha mtoto kwa miezi 6 ya kwanza ya maisha yake.

Baada ya miezi 6, ni vyema kumlisha mtoto vyakula tofauti tofauti, na pia kumnyonyesha ili kuhakikisha kuwa anapata virutubisho anavyostahili ili kuzuia maambukizi ya koo na magonjwa mengine. Mfano wa vyakula vyenye afya ni pamoja na mboga na matunda, (mboga za kijani), maini, mafua ya kupikia ya nazi, maziwa, samaki na mayai.

Maji safi na mazoea ya usafi husaidia kupunguza maambukizi ya koo na magonjwa mengine kama vile kuharisha. Mazoea haya ya usafi yanajumuisha kuosha mboga na matunda, uhakikisha kuwa mahali unapotengenezea chakula ni pasafi, kuosha mikono kwa sabuni na maji au jivu na maji.

NI lazia kila mtoto amalize chanjo zote. Kinga ya mapema ni muhimu; chanjo hizi ni muhimu sana hasa katika mwaka wa kwanza na wa pili. Mtoto atalindwa kutokana na surua, kifaduro, kifua kikuu na magonjwa mengine ya pumu, ambayo husababisha homa ya mapafu.

Wazazi na walinzi wengine wanapaswa kuhakikisha kuwa watoto wavulana na wasichana wanapata lishe bora na chanjo. Wahudumu wa afya pia wanaweza kuwapa wazazi na walinzi habari kuhusu lishe, usafi na chanjo, na jinsi ya kuwalinda watoto kutokana na homa ya mapafu na magonjwa mengine.

Ni rahisi kwa watoto kushikwa na homa ya mapafu na magonjwa mengine ya pumu ikiwa wanaishi katika mazingira yenye moshi. Moshi unaweza kumdhuru mtoto, hata kabla hajazaliwa. Akina mama waja wazito hawafai kuvuta sigara wala kukaa mahali kuna moshi. Hakikisha kuwa watoto wachanga hawakaini ambako kuna moshi na moto. Ni muhimu vijana nao wahimizwa wasivute sigara na pia wawatahadharishe wenzao kuhusu athari za uvutaji sigara.

Moshi una madhara kwa watoto wadogo. Hukaa hewani kwa masaa kadhaa baada ya sigara kuzimwa. Watu ambao hawavuti sigara wanapopumua moshi huu huwa rahisi sana kwao kupata maambukizi ya koo kama vile pumu na saratani.




Sources