Nawezaje kuwazuia watoto wangu kutopata majeraha wanapovuka barabara - Audiopedia
Wakati wa kuvuka barabara watoto wadogo wanafaa kufunzwa:
- wasimame kando ya barabara
- watazame pande zote
- wasikize magari au vyombo vingine vya usafiri kabla ya kuvuka barabara
- washikilie mikono ya mtu mwingine
- wasikimbie ila watembee
- watumie njia za uvukaji kama wako mijini
- wasivuke barabara mahali zimepinda au katikati ya magari yaliyoegeshwa.
- wasivuke barabara ambapo magari yanakwenda kwa kasi
Sources