Nawezaje kupata usaidizi ili niwache kunywa pombe na kutumia mihadarati

From Audiopedia
Jump to: navigation, search

Ni rahisi kuwacha hasa ukipata usaidizi kutoka kwa marafiki.

Ili kuwa mwanachama wa Alcoholics Anonymous (AA), unahitaji kitu kimoja tu: uwe na hamu ya kuwacha kunywa. Unapojiunga na kikundi hiki, mtakuwa na mikutano kila mara na wengine ambao wameacha kunywa pombe, ili muweze kubadilishana matukio yenyu, nguvu na matumaini. Unaweza kuwa na mfadhili - mtu ambaye amewacha kunywa pombe kwa muda, na ambaye anweza kukusaidia. Hakuna malipo yoyote katika AA. Haiungi mkono wala kupinga harakati yoyote, au kuwa na uhusiano wowote na makundi ya kidini au ya kisiasa. Lengo la AA ni kupeleka ujumbe kwa mtu ambaye bado anakunywa pombe na anaumia.

Makundi mengine kama AA yapo kwa ajili ya watu wanaotumia vibaya mihadarati, na kwa familia za watu ambao wanatumia vibaya pombe na mihadarati.

Wewe pia unaweza kuanzisha kikundi chako.

Sources
  • Burns, A. A., Niemann, S., Lovich, R., Maxwell, J., & Shapiro, K. (2014). Where women have no doctor: A health guide for women. Hesperian Foundation.
  • Audiopedia ID: sw010309