Nawezaje kulinda macho yangu

From Audiopedia
Jump to: navigation, search

Nzi hubeba viini. Uso mchafu huvutia nzi, ambao husambaza viini kutoka kwa mtu mmoja hadi mwingine. Ni muhimu kuosha uso na mikono kwa maji na sabuni ili kusaidia kuzuia maambukizi ya macho. Katika maeneo fulani ulimwenguni, mambukizi ya macho husababisha ugonjwa wa 'trachoma', ambao unaweza kusababisha upofu. Ikiwa macho yataambukizwa na kuwa chungu, huenda aliyeathiriwa asiweze kuona, au kuwa kipofu. Ni muhimu kuhakikisha kuwa macho yanasalia yakiwa safi na yenye afya.

Ikiwa macho yako na afya, sehemu nyeupe ya jicho ni safi, macho yako na unyevunyevu na yanang'aa na unaona vizuri usiwe na wasiwasi.

Lakini Ikiwa macho ni makavu kabisa au mekundu, ikiwa kuna uchafu au shida ya kuona, ni vyema kuchunguzwa na mhudumu wa afya haraka iwezekanavyo.

Sources