Nawezaje kuepuka kutumia mihadarati na pombe

From Audiopedia
Jump to: navigation, search

Ili shida hii isitokee tena, ni jambo la muhimu sana kwa mtu kujifunza kukaa mbali na pombe na mihadarati baada ya kuwacha matumizi yake. Njia bora ni kujifunza jinsi ya kukabiliana na matukio maishani. Hili sio jambo rahisi na litachukua muda.

Mwanamke ambaye ametumia pombe na mihadarati kwa njia isiyofaa huona aibu na kujihisi hana nguvu. Ni muhimu afahamu kuwa anaweza kufanya mabadiliko ili kuimarisha maisha yake. Njia moja ni kufanya mabadiliko machache ambayo yataonyesha watu wengine na yeye mwenyewe kuwa anaweza kutatua shida zake.

Hapa kuna mapendekezo ya jinsi ya kufanya mabadiliko:

  • Baada ya kuwacha matumizi ya pombe na mihadarati, anza kula vyakula au vinywaji vyenye afya na wingi wa protini, vitamini na madini. Vyakula hivi huusadia mwili kupona: maini, chachu, mkate uliotengenezwa kwa kutumia nafaka, maharagwe na mboga za kijani. Ikiwa utashindwa kula, basi vitamini zitakusaidia. Tumia tembe ambazo zina vitamini aina B-complex, ambayo ina folic acid.
  • Jiunge na kikundi au tafuta usaidizi mara unapouhitaji. Ni rahisi kutatua shida ikiwa utazungumza na kushirikiana na watu.
  • Jaribu kutatua shida moja baada ya nyingine. Ukifanya hivyo, shida hazitonekana kana kwamba ni kubwa hivi kwamba huweza kuzitatua.
  • Unaweza kumwabia mtu ambaye unamwamini kuhusu mambo ambayo hukupatia wasi wasi, au ambayo hukupatia huzuni au kukukasirisha. Utaanza kuelewa chanzo cha hisia zako na nini unachoweza kufanya kujihisi vizuri tena.
  • Shirikiana na watu kwenye mradi wa kuimarisha jamii yako. Hii itaonyesha kuwa unaelewa umuhimu, na unaweza kuchangia kuleta mabadiliko.
  • Kutana na watu wengine ambao wanafanya kila juhudi kuepuka matumizi ya pombe na mhadarati.
  • Epuka maeneo ambayo yanakupatia shinikizo la kutumia pombe au mihadarati. Shirikiana na wengine kuandaa tamasha za kijamii ambapo pombe au mihadarati haitumiki.


Sources
  • Burns, A. A., Niemann, S., Lovich, R., Maxwell, J., & Shapiro, K. (2014). Where women have no doctor: A health guide for women. Hesperian Foundation.
  • Audiopedia ID: sw010314