Nawezaje hakikisha kuwa napata folic acid folate ya kutosha

From Audiopedia
Jump to: navigation, search

Mwili unahitaji folate kutengeneza cell nyekundu za damu. Ukosefu wa folate waweza sababisha upungufu wa damu kwa wanawake na watoto wachanga. Kwa hivyo kuwa na folate ya kutosha ni muhimu zaidi kwa mwanamke mja mzito.

Unaweza pata folic acid kwa:

  • mboga kama sukuma wiki, spinach, kunde
  • uyoga
  • maini
  • nyama
  • samaki
  • karanga
  • mbaazi na maharagwe
  • mayai

Usipike chakula kwa muda mrefu, kwani huharibu folic acid na vitamin nyingi.

Sources
  • Burns, A. A., Niemann, S., Lovich, R., Maxwell, J., & Shapiro, K. (2014). Where women have no doctor: A health guide for women. Hesperian Foundation.
  • Audiopedia ID: sw010407