Mfumo wa umwagiliaji maji kutoka kwa bomba ni upi
Mfumo wa umwagiliaji maji kwa njia ya matone hufanya kazi sawa na mfumo wa kutumia ndoo lakini umetengenezwa kwa maeneo makubwa zaidi. Badala ya kutumia ndoo, mfumo huu hutumia tangi au pipa la lita 100 hadi 200 au tangi ndogo, linalowekwa mita moja juu ya ardhi ili kuruhusu maji kutiririka chini. Mistari kadhaa hutengezwa, kila moja ikiwa na urefu wa mita 15 hadi 30, na kuunganishwa na njia kuu ya bomba la maji, lilowekwa kwenye shamba au bustani. Bomba kuu hilo hutumika kama chanzo kikuu cha maji, na mabomba mengine hutengezwa kutoka kwa bomba kuu, yakieneza maji katika maeneo yote shamabani. Bomba kuu huwekwa kizibiti ili kudhibiti mtiririko wa maji.
Katika maeneo ambayo mianzi hupatikana kwa urahisi, mirija ya mianzi inaweza kuchukua nafasi ya mabomba ya kawaida ya PVC katika mfumo huo kama chaguo la asili na la gharama nafuu. Mianzi huwekwa kando ya mimea, na mashimo madogo kutengezwa karibu na kila mmea ili kupeleka maji moja kwa moja kwenye mizizi.
Mfumo wa kutumia bomba huweza kumwagilia mimea 500-1000 iliyopandwa na sentimita 30 kati ya safumlalo.Mfumo huu unahitaji takriban lita 100 hadi 200 ya maji kila siku, kulingana na mazao na mazingira. Mfumo huu mkubwa unawafaa wale wanaohitaji kumwagilia eneo kubwa zaidi huku wakihifadhi maji na rasilimali.