Kisima kizuri ni kipi

From Audiopedia
Jump to: navigation, search

Kuna aina nyingi ya visima vya kuteka maji ardhini. Rahisi kati yazo ni shimo la maji lililochimbwa kwa mkono, wakati mwingine huitwa bwawa. Aina ya kisima cha bei ghali zaidi, hujulikana kama kisima cha bomba, ambacho hutumia bomba nyembamba linaloingia ndani kabisa ya ardhi na pampu juu ya kuteka maji.

Kisima kinafaa ikiwa tu watu wanaweza kupata maji kutoka humo. Kisima bora kwa jamii yoyote hutegemea kina cha maji ya chini ya ardhi na rasilimali zinazopatikana kwa kuchimba na kujenga kisima. Katika visa vingi, visima vifupi ambavyo watu huchota maji kwa ndoo vinaweza kuwa bora kuliko visima vya kina vya gharama ambavyo vinahitaji pampu. Visima kadhaa vifupi mara nyingi ni bora kuliko kisima kimoja kirefu, kwa sababu kisima kimoja kikikauka, vingine bado vinaweza kutoa maji.

Kabla ya kuchimba kisima, hakikisha ni kisima bora kwa mahitaji ya kila mtu.


Sources
  • Audiopedia ID: Sw3124