Jinsi ya kuweka maji safi yanayotoka kwa mashimo yaliyowazi
Ili kuboresha maji kutoka kwa shimo la maji lililo wazi, jenga hatua za mawe kwenye shimo la maji ili mtu aweze kuteka maji bila ya kulowekwa. Hakikisha umetumia hatua ya mwisho kavu, kulingana na kiasi cha maji kilichoko kwenye shimo. Kamwe usitembee ndani ya maji., kwani hii inaweza kuleta uchafu na vijidudu na kufanya maji kuwa sio salama.
Chaguo jingine ni kugeuza shimo la maji kuwa kisima kinachofaa kwa kukifunga na matofali au zege. Hii hurahisisha kuteka maji kwa kutumia kamba safi na ndoo, na husaidia kuzuia kisima kutoporomoka au kukauka. Kisima ambacho kimewekwa vizuri kinaweza pia kuhifadhi maji zaidi.
Tafadhali usiwahi kunywa maji moja kwa moja kutoka kwenye shimo la maji. Hakikisha umechuja maji kwa kutumia kitambaa na kuyaacha yatulie kabla ya kunywa ili kuondoa baadhi ya vijidudu. Vilevile, ni bora kuyatibu maji yatokayo kwenye shimo la maji kabla ya kunywa ili kuzuia magonjwa yanayosambazwa na maji.