Jinsi ya kusaidia mchanga kuhifadhi maji kwa wingi

From Audiopedia
Jump to: navigation, search

Ili kuweka udongo wako laini,Ongeza mbolea kwa mchanga,. Hii huboresha mchanga kuhifadhi maji. Unapochaganya mbolea husaidia mchanga kukaa na unyevu kwa muda mrefu, na kupea mimea yako nafasi nzuri ya kupitiza maji inavyohitajika.

Njia nyingine muhimu ni kufunika mchanga kwa kutumia matandazo. Matandazo yanaweza kuwa kitu chochote kama vile majani, nyasi kavu, au majani ya mazao ya zamani. Unapotandaza matandazo juu ya mchanga husaidia kuweka mchanga na unyevu, kwa sababu huzuia maji kukauka na kutoweka hewani. Pia hufanya mchanga kupitiza hewa na kuulinda kutokana na jua kali. Hii ni muhimu sana wakati wa kiangazi au wakati mvua haitoshi.

Waweza pia kupanda mazao ya kufunika, kama vile nyasi au kunde, kumea kwa mchanga wakati huvuni mazao yako makuu. Mazao ya kufunika hufanya mchanga kuwa laini kwa kupunguza kasi ya mtiririko wa maji ya mvua na kuyazuia yasitirike. Mazao ya kufunika pia huongeza manyua kwenye mchanga, na kufanya mchanga kuwa bora zaidi katika kuhifadhi maji.

Katika maeneo ambayo mvua nyingi hunyesha kwa wakati mmoja, ukulima wa bila kuchimba mchanga unaweza kusaidia. Badala ya kuchimba ardhi, unaacha mabaki ya mazao juu. Majani yaliyo kauka hufunika na husaidia maji ya mvua kuingia kwenye ardhi polepole. Hii, Husaidia maji kutokauka na kutoweka hewani na kuweka mchanga na unyevu kwa muda mrefu.


Sources
  • Audiopedia ID: Sw3105