Jinsi ya kujenga kisima salama
Visima vinaweza kuwa chanzo kizuri cha maji, lakini vinahitaji kutunzwa ili kuzuia uchafuzi. Kisima kilichotunzwa huwa ni shimo lililochimbwa kwa mkono na bitana, kifuniko cha zege, chombo cha kuinua maji, na mifereji ya maji. Kila moja ya vifaa hivi husaidia kulinda kisima. Vyote vikiwapo, na utunzaji imara wa maji, kisima cha familia kinaweza kuwa salama zaidi.
Kwa hivyo visima havipaswi kuchimbwa karibu sana na maeneo kama vile vyoo vya shimo, mabomba ya maji taka, shimo la uchafu au maeneo ambayo mifugo hufugwa. Maeneo haya yanaweza kuruhusu vijidudu hatari kuingia ndani ya maji. Ni muhimu kuweka visima umbali wa angalau mita 30 kutoka kwa vyanzo hivi ili kuhakikisha maji yanabaki safi na salama kwa kunywa.
Visima vifupi kwa mara nyingi huwa katika hatari ya kukauka haraka au kuchafuliwa, haswa wakati wa mvua. Maji ya mvua yanaweza kubeba uchafu, vijidudu, na vichafuzi vingine ndani ya kisima. Watu na wanyama wanaweza pia kuleta vijidudu wakitembea, ndoo chafu na kamba zinaweza kuhamisha vijidudu kwenye maji. Ili kuepuka haya, ndoo safi tu na kamba zinapaswa kutumika.
Katika mchanga mgumu sana, kuweka kizuizi kwa kisima kunaweza kuonekana kuwa sio lazima. Lakini ni vyema kuweka kizuizu cha angalau mita 1 hadi 2 chini ya ardhi ili kuzuia kuta za kando kuanguka. Ikiwa kisima kizima kimekingwa kitafanya chanzo cha maji kutegemewa zaidi, lakini itakuwa vigumu zaidi kuchimba kisima zaidi baadaye. Kisima kinaweza kukingwa kwa kutumia mawe au miamba, kwa matofali ya moto, au kwa saruji.
Ili kulinda kisima zaidi, zingira eneo karibu na juu ili kuzuia maji machafu yasitiririkie ndani. Unaweza pia kutengeneza jukwaa dogo la mifereji ya maji kuzunguka juu kwa kutumia matofali au zege. Jukwaa hili hubeba maji kutoka kisimani hadi eneo la mifereji ya maji na huzuia eneo karibu na kisima kupata tope, na kuzaliana vijidudu na wadudu. Vidudu vinaweza kukua katika nyufa, kwa hiyo ni muhimu kwamba jukwaa limetengenezwa vizuri. Mimina saruji kwa kina cha milimita 75, na ukingo wa nje ulioinuliwa milimita 150 juu. Jukwaa zima na juu ya jukwaa unapaswa kuimarishwa na waya ya milimita 3 ili kuzuia kupasuka. Chini ya jukwaa, unaweza kupanda mboga ili kufaidika na maji yanayotiririka.
Funika kisima angalau kwa pipa au kifuniko ili kuzuia watoto, uchafu na wanyama kuanguka ndani ya kisima. Bamba la kifuniko cha zege ni bora zaidi kulinda kisima chako.