Jinsi ya kuangalia iwapo mchanga wako unanyonya maji vizuri

From Audiopedia
Jump to: navigation, search

Ili kukuza mimea iliyo na afya, mchanga huhitaji kunyonya maji haraka na kuwekeza maji. Iwapo maji yanakaa tu juu ya mchanga au kukosa kuwekeza maji vilivyo, hii inamaanisha kuwa mchanga huo sio bora kwa upanzi. Njia rahisi ya kuangalia jinsi mchanga unavyopitiza maji ni kwa kupima kiwango cha maji kupenyeza katika mchanga. Unaweza kufanya Jaribio hili kwa urahisi nyumbani, na utahitaji vitu vichache tu: chupa za plastiki, mchanga kutoka kwa shamba lako, na maji safi.

Kwanza, chukua chupa chache za plastiki zilizo angavu au na uwazi. Kisha Kata sehemu za chini za chupa na uondoe vifuniko. Weka chupa ikiangalia juu chini kwenye safu ya mchanga. Ikiwa chupa hizo hazitasimama zenyewe, tumia mawe kuzisimamisha. Kisha, chukua sampuli za udongo kutoka sehemu mbalimbali za shamba lako. Weka kila sampuli ya udongo kwenye mfuko tofauti, halafu vunja mchanga vipande vidogo. Ukishafanya hivyo jaza mchanga wa sampuli yako nusu chupa. Baada ya hayo, mimina maji safi ndani ya chupa polepole hadi mchanga uloweke. Hii inamaanisha kuwa mchanga hauwezi kuchukua maji zaidi na umejaa.Baada ya mchanga kulowekwa, mimina maji kiasi an uwacha yatiririke. Tumia saa ili kupima muda wa maji kupita kwenye mchanga.

Iwapo maji yatapita kwa haraka kwenye mchanga, ni ishara nzuri. Hii, inamaanisha kuwa mchanga wako uko na muundo mzuri na nafasi nzuri ya hewa na maji. Mchanga unaonyonya maji kwa haraka mara nyingi huwa na udongo mwingi hivyo basi maji huteremka kwenye mchanga haraka, na kupunguza uwezekano wa maji ya mvua kutiririka kwenye vijito au maziwa yaliyo karibu.

Ikiwa maji yatachukua muda mrefu kupita kwenye mchanga, inaweza kumaanisha kuwa mchanga umegandamizwa. Mchanga ulioshikana hauna nafasi ya kutosha ya kupitisha hewa na maji, hivyo kufanya mchanga kuwa mgumu na kusababisha mimea kutomea. Pia hili linaweza kutokea ikiwa hakuna viumbe hai vya kutosha kama minyoo kwenye mchanga. Kiwango cha upenyezaji wa maji kinaweza kufanya iwe vigumu kwa maji ya mvua kuingia ndani vizuri na inaweza kusababisha maji mengi kusambaa badala ya kukuza mimea yako.


Sources
  • Audiopedia ID: Sw3104