hedhi huwa nzito ikiwa sodo au kitambaa unachotumia kitalowa katika muda wa lisaa limoja.
hedhi pia ni ndefu ikiwa itaendelea kwa muda wa zaidi ya siku nane.
hedhi ikitoka na kufanana kama vipande vidogo vya maini, hii ni ishara ya hedhi nzito.
hedhi inayoendelea kwa wiki kadhaa, miezi au miaka husababisha shida ya upungufu wa damu mwilini.
Sababu zinazokisiwa.
Huenda homoni haziko sawa kwa hivyo ovari haitoi yai. Hii ni kawaida kwa wanawake chini ya umri wa miaka 20 na wanawake wa umri zaidi ya 40.
Huenda mbinu ya kupanga uzazi iliyotiwa tumboni inasababisha hedhi nzito.
Kuharibika kwa mimba, hata kama hukujua kuwa wewe ni mja mzito.
Ikiwa una maumivu tumboni pamoja na kuvuja damu, huenda umeshika mimba na haiko mahali inastahili kuwa kwenye mshipa tumboni. TAHADHARI. Nenda hospitalini mara moja.
Huenda pia una shida ya mshipa wa tezi.
Huenda una shida ya mojawapo ya 'fibroids' au 'polyps' au saratani tumboni.
TAHADHARI: Ikiwa hedhi yako ni nzito, muone mhudumu wa afya ambaye amepata mafunzo ya jinsi ya kukagua sehemu za uzazi, na ikiwa:
damu inavuja sana kutoka sehemu yako ya uzazi. .
hedhi yako imekuwa nzito na kukaa kwa muda, katika kipindi cha miezi 3.
unafikiri kuwa wewe ni mja mzito.
unapata maumivu makali pamoja na hedhi yako.
Sources
Burns, A. A., Niemann, S., Lovich, R., Maxwell, J., & Shapiro, K. (2014). Where women have no doctor: A health guide for women. Hesperian Foundation.