Kwa vile watu wa familia moja hushirikiana kwa karibu, ni rahisi sana kusambaza viini na magonjwa kwa familia nzima.
Familia haitakuwa na maambukizi ikiwa:
wataosha vyombo wanavyotumia kwa kula kwa sabuni (au kwa kutumia jivu) na maji masafi baada ya kuvitumia. Ikiwezekana, waviache vyombo hivi vikauke kwenye jua (jua huua viini vinavyosababisha magonjwa).
wasafishe nyumba kila mara. Wafagie na kuosha sakafu zote, kuta na chini ya viti. Wazibe nyufa na mashimo kwenye sakafu au kuta, ambapo mende, kunguni na nge hujificha.
anika malazi kwenye jua ili kuua vijidudu na kunguni.
usiteme mate sakafuni. Funika mdomo kwa kutumia mkono wako au kitambaa cha mkononi unapokohoa au kupiga chafya. Ikiwezekana, osha mikono yako.
Sources
Burns, A. A., Niemann, S., Lovich, R., Maxwell, J., & Shapiro, K. (2014). Where women have no doctor: A health guide for women. Hesperian Foundation.