Je ni mifumo ipi mingine ya unyunyizaji maji shambani ya gharama nafuu
Unyunyizaji maji kwa kutumia nyungu ndogo kisha kuweka ardhini ni njia nyingine ya kitamaduni inayotumika. Mfumo huu hutumia nyungu au vyombo vya udongo ambavyo huchimbiwa mashimo na kuwekwa shimoni kando ya mimea. Vyungu hivi hujazwa maji na kufunikwa na kifuniko au jiwe. Kuta za vyungu hivyo huruhusu maji kutoka polepole, hadi kwa mizizi. Jamii ambazo huenda hazina vyungu vya udongo, maganda ya matunda magumu kama vile passioni hukaushwa kishwa mashimo kuwekwa na kutumika kama njia nyingine mbadala. Njia hii hutoa unyevu thabiti moja kwa moja hadi kwa mizizi na kupunguza uvukizi na kupoteza maji.
Unyunyizaji maji kwa kutumia chupa pia ni mojawapo ya mbinu rahisi na ya gharama nafuu. Chupa ya plastiki hujazwa maji na kuwekwa juu chini kwenye mchanga karibu na mmea. Udongo mnene huzuia maji kutoka kwenye chupa mara moja. Maji yanapotoka polepole , yanatiririka moja kwa moja hadi kwenye mizizi ya mmea. Njia hii huzuia maji kupotea na kufanya maji kupatikana kwa mmea kwa muda mrefu, na kuweka udongo kuwa na unyevu na kusaidia ukuaji wa mimea kwa kutumia maji kidogo.