Je Unyunyizaji maji shambani uko na faida gani

From Audiopedia
Jump to: navigation, search

Mfumo wa kunyunyiza maji shambani ni mojawapo ya njia bora zaidi za kukuza mimea.

Tofauti na mbinu zingine za unyunyizaji maji ambazo hunyunyizia maji juu ya eneo kubwa, au mafuriko, mfumo wa unyunyizaji maji hupeleka maji moja kwa moja kwenye msingi wa kila mmea. Njia hii iliyolengwa ya kumwagilia maji hupunguza upotevu wa maji kwa sababu mimea pekee ndiyo inayopokea maji, badala ya udongo unaouzunguka. Hivyo basi unyunyizaji maji wa aina hii hutumia maji chini ya asilimia 30 hadi 50 kuliko mbinu za jadi, na husaidia kuhifadhi rasilimali hii muhimu. Katika maeneo ambayo usambazaji wa maji ni mdogo sana, kunaweza kusiwe na akiba halisi ya maji, lakini badala yake kuongezeka kwa uzalishaji ukitumia kiwango sawa cha maji kama cha hapo awali. Katika maeneo yaliyo na ukame sana au kwenye mchanga mwingi, siri ni kunyunyiza maji polepole iwezekanavyo. Ratiba ya umwagiliaji maji inaweza kutengezwa kwa usahihi ili kukidhi mahitaji ya mazao, na ongezeko bora la mavuno.

Unyunyizaji maji hupatia mimea maji kidogo ya kutosha, ambayo hutengeza mazingira bora ya ukuzaji mimea. Mbinu hii pia husaidia uotaji bora wa mbegu, huongeza mavuno ya mazao, na kupunguza ukuaji wa magugu. Kwa kuwa maji huenda moja kwa moja kwenye mimea, magugu hayana nafasi ya kumea kwa urahisi. Vilevile, unyunyizaji maji unaweza kuondoa magonjwa mengi yanayosambazwa kwa kuchanganyikana maji na majani.

Faida nyingine ni kwamba unyunyizaji maji shambani hupunguza uharibifu wa maji, hivyo basi virutubisho vichache hupotea kutoka kwa mchanga. Mbolea zinazotumiwa kupitia mifumo ya unyunyizaji maji hufikia mizizi ya mimea moja kwa moja, kwa hiyo hutumiwa kwa ufanisi bora. Hii haiokoi pesa tu bali hupunguza uchafuzi wa mazingira kwani ni mbolea kidogo tu inayochanganyikana na maji ya chini ya ardhi.

Kwa ujumla, kutumia mfumo wa kunyunyiza maji shambani hupunguza gharama za ukulima, huongeza uwezo wa mchanga kuhifadhi maji, na huweka mbolea kando na maji yapatikanayo ardhini, na kuifanya kuwa njia bora ya kunyunyizia mimea maji.


Sources
  • Audiopedia ID: Sw3111